Ataamka kutoka thiyeta baada ya ´Aswr

Swali: Mtu ambaye anataka kufanya operesheni wakati wa Dhuhr. Anajua kuwa atatoka thiyeta wakati ´Aswr na Maghrib imeshatoka. Je, akusanye ´Aswr na Dhuhr wakati wa Dhuhr na Maghrib na ´Ishaa wakati wa ´Ishaa?

Jibu: Ndiol, anaweza kufanya hivo. Bali ni wajibu kwake kufanya hivo. Ikiwa atafanyiwa operesheni baada ya kwamba kumeshaingia wakati wa swalah ya kwanza na operesheni hiyo itaendelea mpaka utoke wakati wa ile swalah ya pili, basi anatakiwa ajumuishe katika ile swalah ya kwanza. Ikiwa atafanyiwa operesheni kabla ya kuingia ile swalah ya kwanza, basi anuie kuchelewesha swalah hiyo ya kwanza na aikusanye pamoja na ile ya pili wakati wa ile swalah ya pili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Källa: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 18/10/2017