Aswali Maghrib na ´Ishaa


Swali: Kuna mwanamke ametwahirika wakati wa ´Ishaa. Je, analazimika kuswali Maghrib?

Jibu: Ndio, anatakiwa kuswali Maghrib na ´Ishaa katika moja ya maoni ya wanazuoni. Wako wanazuoni wengine wenye kuona kuwa anatakiwa kuswali ´Ishaa peke yake. Maoni ya karibu zaidi ni kwamba aswali Maghrib na ´Ishaa. Kwa  sababu ni swalah mbili ambazo moja inakusanywa na nyingine. Vivyo hivyo endapo atasafika kabla ya Maghrib, basi atatakiwa kuswali Dhuhr na ´Aswr.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (23)
  • Imechapishwa: 28/01/2022