Msingi wa vichinjwa katika miji ya waislamu ni halali


Swali: Ni upi msingi juu ya nyama; ni uhalali au uharamu?

Jibu: Msingi ni uharamu. Vichinjwa msingi ni uharamu. Lakini vinavyochinjwa katika miji ya waislamu, msingi ni uhalali. Vinavyochinjwa na kuuzwa katika masoko ya waislamu, msingi ni uhalali mpaka pale utapojua kuwa ni haramu au imechinjwa kwa njia isiyokuwa ya Kishari´ah. Vinginevyo msingi juu ya vinavyochinjwa katika miji ya waislamu ni uhalali na wewe huna juu yako kitu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (61) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13585
  • Imechapishwa: 16/11/2014