Asli ya chimbuko la waarabu na mayahudi

Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni katika kizazi cha Ismaa´iyl. Allaah alimruzuku Ibraahiym (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) wavulana wawili; wa kwanza ni Ismaa´iyl ambaye mama yake ni Haajara. Ismaa´iyl alikuwa ni Nabii na katika kizazi chake ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwana wa pili alikuwa ni Ishaaq ambaye alikuwa mtoto wa Saarah ambaye alikuwa ni binamu yake. Ishaaq alikuwa ni Nabii pia. Allaah alimruzuku Ya´quub. Ya´quub alikuwa ni Israa´iyl. Manabii wote wa wana wa Israa´iyl walikuwa wanatokamana na kizazi cha Ya´quub. Miongoni mwao ni Muusa – na ndiye Mtume wa kwanza wa wana wa Israa´iyl – halafu wakafuatia wengine baada yake. Miongoni mwao kuna Zakariyyah, Yahyaa, Sulaymaan na Daawuud mpaka Allaah alipowakhitimishia kwa ´Iysaa. Kwa hivyo Manabii wa wana wa Israa´iyl wote wanatokamana na kizazi cha Ishaaq. Ni wana wa Israa´iyl. Upande mwingine katika kizazi cha Ismaa´iyl ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah, uk. 85-86
  • Imechapishwa: 30/04/2020