Asli ni kuwa kichinjwa kinatajiwa jina la Allaah

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Tajeni jina la Allaah na mle.”

Si ni dalili inayofahamisha kuwa nyama inakuwa halali baada ya kutaja jina la Allaah?

Jibu: Hapana. Katika hali hii ni kutajwa kwa jina kwa ajili ya chakula, ni kama mfano wa:

“Taja jina la Allaah na ule kwa mkono wako wa kuume.”

Ni kwa ajili ya chakula. Hukulazimishwa kupeleleza kama watu katika mji wanataja jina la Allaah [wakati wa kuchinja]. Asli ni kuwa kichinjwa kinatajiwa jina la Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (42) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighastah%20%20-%2011%20-%201%20-%201437.mp3
  • Imechapishwa: 14/03/2017