Swali: Mimi ni askari na nimekutana na mwezi wa Ramadhaan. Je, inajuzu kwangu kula pamoja na kuzingatia kwamba hali yangu hainisaidii juu ya suala la funga?

Jibu: Haijuzu kwako kula katika Ramadhaan ilihali swawm ni yenye kukuwajibikia. Isipokuwa ukiwa ni msafiri au mgonjwa maradhi ambayo huwezi kufunga. Amesema (Ta´ala):

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Atakayekuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi katika siku nyinginezo.”[1]

وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ

“Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika dini.”[2]

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

”Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[3]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninapokuamrisheni jambo basi lifanyeni kwa kiasi cha uwezo wenu.”

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah al-Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

[1] 02:185

[2] 22:78

[3] 02:286

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daa’imah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Ladjnah ad-Daa’imah (3924)
  • Imechapishwa: 27/04/2020