Swali: Maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah ataziweka mbingu kwenye kidole.”

Je, tumthibitishie Allaah kuwa na kidole kutokana na Hadiyth hii?

Jibu: Na je wewe una mashaka juu ya hili? Ndio. Yule asiyethibitisha kidole ni Mu´attwil. Hili limesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vilevile hili limetajwa katika Tawraat. Kuna myahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kumuuliza juu ya hilo na akamsadikisha na akapendekezwa na hili na akacheka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka magego yake yakaonekana kwa kuwa ni katika mambo alosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1427-2-13.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020