Swali: Akifa ambaye alikuwa haswali atapata uombezi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au uombezi wa watoto wake waliokufa wakiwa wadogo?

Jibu: Mwenye kufa ilihali ni mwenye kuacha Swalah kwa kukusudia, huyu sio Muislamu na hapati uombezi wowote.

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ

“Basi hautowafaa uombezi wowote [ule] wa waombezi.” (74:48)

مَا سَلَكَكُمْ فِي سَقَرَ قَالُوا لَمْ نَكُ مِنَ الْمُصَلِّينَ

“Nini kilichokuingizeni katika [Moto wa] Saqar?” Watasema: “Hatukuwa miongoni mwa wanaoswali.” (74:42-43)

Mpaka Aliposema (Ta´ala):

فَمَا تَنفَعُهُمْ شَفَاعَةُ الشَّافِعِينَ

“Basi hautowafaa uombezi wowote [ule] wa waombezi.” (74:48)

Ambaye haswali kwa kukusudia, na akafa juu ya hali hiyo, hautomfaa uombezi wa waombezi na haijuzu kumuombea msamaha wala kumuombea du´aa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (11) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_11.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2018