Asiyemwamini Muhammad (´alayhis-Salaam) hamwamini ´Iysaa vilevile

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema mnaswara fulani ambaye yuko katika Dini ya ´Iysaa ni sahihi kwa kuwa inahusiana na kumuabudu Allaah Mmoja asiyekuwa na mshirika.

Jibu: Ambaye yuko katika Dini ya ´Iysaa sahihi anamwamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa kuwa ´Iysaa alibashiria kuhusu Muhammad:

وَمُبَشِّرًا بِرَسُولٍ يَأْتِي مِن بَعْدِي اسْمُهُ أَحْمَدُ

“… na mwenye kubashiria kuja kwa Mtume baada yangu jina lake: “Ahmad.” (61:06)

Hii ni khabari ya ´Iysaa (´alayhis-Salaam) kuhusu Muhammad. Anayemwamini ´Iysaa kikweli, basi anamfuata Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa hakumuamini Muhammad, basi ni mwenye kumkanusha, Muhammd na wajumbe wengine wote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-01-27.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014