Asiyefanya sababu hatopata rehema za Allaah


Swali: Kuna ndugu mmoja amesema “Mimi naingia Peponi kwa ajili ya rehema za Allaah tu, matendo ni kwa ajili ya kupandishwa daraja Peponi”. Je, kauli hii ni sahihi?

Jibu: Utaingia Peponi kwa ajili ya rehema za Allaah. Lakini matendo ni sababu, ewe ndugu. Fanya sababu ili upate rehema. Ikiwa hukufanya sababu hutopatwa na rehema. Unasema “Mimi Allaah atanirahamu” kisha hufanyi sababu? Hapana, hili haliwezekani. Matendo ni sababu na kuingia Peponi ni kutokana na rehema za Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (62) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13740
  • Imechapishwa: 16/11/2014