Asiyeamini ujuu wa Allaah ni Fir´awn mkanushaji

Maalik bin Anas amesema:

“Allaah yuko juu ya mbingu na ujuzi Wake uko kila mahali.”

Ibn-ul-Mubaarak aliulizwa ni vipi tutamtambua Mola wetu. Akasema:

“Kwamba Yuko juu ya mbingu na juu ya ´Arshi Yake na ametengana na viumbe Wake.”

Hayohayo yamesemwaa na Ahmad bin Hanbal. ash-Shaafi´iy amesema:

“Ukhaliyfah wa Abu Bakr Allaah kauhukumu juu ya mbingu na akazikusanya nyoyo za mawalii Wake.”

Mwenye kuamini kwamba Allaah yuko ndani ya mbingu na amefupika na zimemzunguka na kwamba ni mwenye kuhitajia ´Arshi au kiumbe kingine au kwamba kuwa Kwake juu ya ´Arshi kama ambavyo kiumbe anavyokuwa juu ya kiti chake, ni mpotevu na mzushi mjinga.

Mwenye kuamini kwamba mbinguni hakuna mungu anayeabudiwa na kwamba juu ya ´Arshi hakuna mungu anayeswaliwa na kusujudiwa na kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupandishwa kwa Mola Wake na kwamb Qur-aan haikuteremshwa kutoka Kwake, basi huyo ni Fir´awn mkanushaji. Kwani Fir´awn ndiye ambaye alimkadhibisha Muusa pindi alipomwambia kwamba Mola wake yuko juu ya mbingu:

وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا هَامَانُ ابْنِ لِي صَرْحًا لَّعَلِّي أَبْلُغُ الْأَسْبَابَ أَسْبَابَ السَّمَاوَاتِ فَأَطَّلِعَ إِلَىٰ إِلَـٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ كَاذِبًا

“Fir’awn akasema: “Ee Haamaan nijengee mnara ili nifikie njia; njia za mbinguni ili nimchungulie Mungu wa Muusa, kwani hakika mimi namdhania ni mwongo.” [1]

Upande mwingine Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimsadikisha Muusa na akathibitisha kuwa Mola wake yuko juu ya mbingu. Usiku ule wa safari ya usiku alipandishwa kwa Allaah. Mola wake akamfaradhishia swalah khamsini. Akataja namna alivyorudi kwa Muusa ambaye alimwambia arejee kwa Mola wake na amuombe apunguze kwa ajili ya Ummah wake. Hadiyth iko katika vitabu Swahiyh. Kwa hivyo yule mwenye kuafikiana na Fir´awn na akampinga Muusa na Muhammad ni mpotevu. Yule mwenye kumfananisha Allaah na viumbe ni mpotevu. Yule mwenye kukanusha kitu ambacho Allaah amejisifu kwacho ni kafiri.

[1] 40:36-37

  • Mhusika: Imaam Swiddiyq Hasan Khaan al-Qanuujiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qatwf-uth-Thamar, uk. 48-49
  • Imechapishwa: 21/12/2018