Swali: Inafaa kuswali nyuma ya mtu Suufiy ambaye analingania katika madhehebu yake, anasherehekea mazazi na anasema kuwa Shiy´ah ni ndugu zetu?

Jibu: Haifai kumteua mtu kama huyu kuwa imamu. Lakini akiwa ameshateuliwa kuwa imamu na hakuna mwengine badala yake, basi utatakiwa kuswali nyuma yake badala ya kuswali peke yako. Swali pamoja naye na wala usiache swalah ya mkusanyiko.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (11) http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/14466
  • Imechapishwa: 10/10/2017