Ashaa´irah wanamfuata Ibn Kullaab na sio Abul-Hasan al-Ash´ariy

Swali: Imaam Abul-Hasan al-Ash´ariy (Rahimahu Allaah) alikufa juu ya Salafiyyah na juu ya ´Aqiydah sahihi?

Jibu: Allaah akitaka. Aliweka wazi hili ya kwamba anafuata madhehebu ya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) na kwamba amejirudi katika yale aliyokuwemo. Haya yanapatikana katika vitabu vyake vya mwisho alivyoandika.

Wale wanaosema kuwa ni ´Ashaa´irah na Ash´ariyyah hawamfuati Abul-Hasan al-Ash´ariy. Wanafuata madhehebu ya Ibn Kullaab. Ni Kullaabiyyah[1]. Sio ´Ashaa´irah. Kwa sababu Abul-Hasan al-Ash´ariy jambo lake la mwisho amekufa juu ya ´Aqiydah ya Imaam Ahmad. Alisema hilo wazi.

[1] Tazama https://firqatunnajia.com/21-maneno-ya-allaah-subhaanahu-wa-taala/

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17356
  • Imechapishwa: 10/12/2017