Ashaa´irah hawathibitishi Allaah kuwa juu ya mbingu na kulingana Kwake juu ya ´Arshi. Wanamzingatia yule mwenye kuthibitisha sifa ya Allaah kuwa juu na kulingana Kwake juu ya ´Arshi kwamba ni Mujassimah na Mushabbihah. Haya ni tofauti ni yale waliyomo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Kwani wao wanathibtiisha Allaah kuwa juu na kulingana kama alivyojielezea Allaah (Subhaanah) Mwenyewe na akamsifu hivo Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na kumfanyia namna wala makanusho.

Salaf wengi wameweka wazi kwamba yule asiyethibitisha ujuu na kulingana kwa Allaah ni kafiri. Ashaa´irah wameafikiana na Jahmiyyah katika kukanusha sifa hii. Lakini hata hivyo Jahmiyyah wanaonelea kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) yuko kila mahali na wanaitwa Huluuliyyah. ´Ashaa´irah wanasema kwamba Allaah alikuwepo pasi na mahali na kwamba hivi sasa yuko mahali kabla ya kuumba mahali.

Ashaa´irah wanaafikiana na Ahl-us-Sunnah kwamba waumini watamuona Mola wao Peponi. Kisha wanasema kwamba maana ya uonekanaji ni ziada ya elimu ambayo ataiumba Allaah kwenye moyo wa yule mtazamaji. Wanamaanisha kwamba sio uonekanaji wa kikweli wa macho. Kwa hayo wanapinga uonekanaji ambao umethibitishwa na Qur-aan na kumekuja Hadiyth zilizopokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayh wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan Abaa Butwayn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Rasaa-il wal-Masaa-il an-Najdiyyah (2/177)
  • Imechapishwa: 11/03/2019