Swali: Ni ipi hukumu ya kuangalia filamu ”ar-Risaalah” (The Message) ambapo watu wanaweza kujifunza maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa njia nyepesi sana?

Jibu: Kamwe kabisa. Ndani yake hakuna kujifunza wasifu. Ndani yake kuna kujifunza ukafiri na uzandiki. Filamu ya ”ar-Risaalah” na nyenginezo mfano wake ambazo zinamzungumzia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na nyenginezo kuhusu jukumu la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake na filamu nyenginezo zote ni haramu kabisa. Haijalishi kitu ikiwa zitaitwa kuwa ni ”filamu za Kiislamu”, ”filamu za maigizo”, ”filamu za mapenzi”, ”filamu za mahaba” na kadhalika. Zote hizo ni haramu na zote ni wongo na zote ni udajali. Pesa zinazotokamana nazo ni haramu na kununua kaseti zake ni haramu.

Aidha ni haramu pia kutazama chaneli ya ”ar-Risaalah” na ”at-Twuyuur-ul-Jannah” kwa sababu zimejengeka juu ya uzushi, ukhurafi, muziki na uchache wa haya juu ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=FN_yDDbCf10&t=0s
  • Imechapishwa: 07/02/2021