Kwa sababu muheshimiwa Shaykh Ibn Baaz amenusuru ´Aqiydah ya kwamba Allaah amelingana juu ya ´Arshi na kujuzisha kuuliza swali la kwamba Allaah yuko wapi katika taaliki yake ya “Fath-ul-Baariy”[1], as-Saqqaaf akamweleza kwa njia ifuatayo:

“Maneno ya aliyefanya taaliki yatupiliwe mbali. Kwa sababu haijui Tawhiyd. Alitakiwa kuona haya ambaye anawalingania watu katika ´Aqiydah ya kwamba Allaah yuko juu ya mbingu na atubie.”

Kwa ujumla ni kwamba mtu huyu ni Jahmiy kindakindaki. Anapinga maana ya Aayah zinazozungumzia sifa za Allaah kwa njia ya kuzipindisha maana na kuzikanusha, kama alivofanya kwa Aayah zinazozungumzia kulingana/kuwa juu. Vilevile anazipinga Hadiyth ambazo ni Swahiyh zinazozungumzia sifa za Allaah na kudai kwamba ni dhaifu na matokeo yake akaenda kinyume na wanachuoni wa Hadiyth na wa kujeruhi na kusifu. Kwa mfano amefanya hivo juu ya Hadiyth hizi na nyenginezo nyingi mfano wake. Anadhoofisha Hadiyth isemayo:

“Nimemuona Mola wangu katika umbile zuri kabisa.”

na anawazulia uongo baadhi ya maimamu pindi anapotaja vyanzo vyake na hukumu. Kama ambavo anadhoofisha Hadiyth kuhusu mikono, mshiko, vidole, kucheka na sifa nyenginezo. Huenda baadhi ya ndugu zetu wakamtengea muda na wakawafichulia watu ujinga wake, ujinga wake na aibu zake na Allaah awasalimishe waislamu kutokamana na shari zake.

[1] 1/188.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/1/11-12)
  • Imechapishwa: 26/04/2019