Swali: Je, ar-Rashiyd na al-Haafidhw ni katika Majina ya Allaah?

Jibu: Sijasikia haya. Kunasemwa ya kwamba Allaah ni Haafidhw.

فَاللَّـهُ خَيْرٌ حَافِظًا

“Basi Allaah ni Mbora wa wenye kuhifadhi.” (12:64)

اللَّـهُ حَفِيظٌ عَلَيْهِمْ

“Allaah ni Mhifadhi wao.” (42:06)

Kunasemwa kuwa Allaah ni Haafidhw. Ama kusema kuwa ni Jina sijui lolote kuhusu hilo.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com