ar-Raajihiy maoni yanayosema kufanya Tayammum juu ya swalah ya jeneza

Swali: Je, swalah ya jeneza imeshurutisha yale yaliyoshurutishwa katika swalah ya kawaida katika twahara, kuelekea Qiblah na mengineyo?

Jibu: Ndio, kwa sababu ni swalah. Ni lazima kuelekea Qiblah na ni lazima kuwa na wudhuu´. Haitoshi kufanya Tayammum kwa kuchelea jeneza litaondoka. Kuna maoni dhaifu yanayosema kwamba mtu afanye Tayammum akichelea kuondolewa kwa jeneza. Lakini hata hivyo ni maoni yasiyokuwa na nguvu. Maoni ya sawa ni kwamba swalah ya jeneza haisihi isipokuwa mpaka mtu atawadhe ikiwa anapata maji. Ikiwa hakupata [udongo wa kufanya] Tayammum akiwa nje ya mji [ni sawa]. Ama ndani ya mji ni lazima atawadhe. Mfano wa hilo ni swalah ya ijumaa akichelea kumpita. Ni lazima kutawadha japokuwa muda utampita na hapo itambidi aswali Dhuhr.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (10) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191426#219753
  • Imechapishwa: 21/05/2019