ar-Raajihiy kutundika Aayah za Qur-aan ukutani na mazulia yaliyo na Ka´bah

Swali: Ni ipi hukumu ya kutundika Aayah kwenye ukuta? Ni ipi hukumu ya kutundika picha ya Ka´bah au jiwe la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au picha ya jiwe jeusi? Je, mtu anaweza kusema kuwa haya ni matendo ya Suufiyyah?

Jibu: Kuhusu kutundika Aayah wanachuoni wa leo wamelizungumzia hilo. Wako ambao wameonelea kuwa lachukiza. Wako wengine ambao wameonelea kuwa lajuzu. Bora zaidi ni kutofanya hivo. Kwa sababu Qur-aan inasomwa na kufanyiwa ´ibaadah kwa kisomo chake. Haitundikwi.

Wako wengine ambao wamesema hakuna hakuna neno kutundika baadhi ya Aayah. Kwa hiyo jambo katika haya ni pana. Lakini vile ninavyoonelea mimi ni kwamba bora zaidi ni mtu kuacha kufanya hivo.

Kuhusu kutundika picha ya Ka´bah sioni kama kuna ubaya kwa kufanya hivo. Isipokuwa tu kiwa kama kunakhofiwa baadhi ya watu wasije kuibusu, kama walivyofutu baadhi ya wanachuoni wa kamati la wanachuoni wakubwa. Wanaonelea kuwa haitakikani kwa mtu kuweka mazulia/mikeka iliyo na Ka´bah. Kwa sababu baadhi ya watu wanadhani kuwa inabusiwa picha hii.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/431/431.mp3
  • Imechapishwa: 01/07/2018