ar-Raajihiy kuhusu ujinga ni udhuru 03

Swali: Je, inafaa kumkufurisha mtu kwa dhati yake pindi anapofanya moja katika mambo yanayochengua Tawhiyd kama kwa mfano akamwomba au kutaka uokozi wa haraka kutoka kwa mwengine asiyekuwa Allaah kwa kudhani kuwa yule anayemwomba au anayemuwekea nadhiri ni mtu ambaye ana cheo cha juu mbele ya Allaah na kufikiri kuwa inafaa kumwomba uombezi mbele ya Allaah?

Jibu: Haijuzu kukufurisha isipokuwa baada ya kusimamisha hoja. Mtu huyo anatakiwa kubainishiwa. Akiendelea baada ya ubainifu basi hapo ndipo atahukumiwa kuwa ni kafiri. Lakini kabla ya hapo pengine akawa ni mjinga. Pengine ni mwenye ufahamu wa kimakosa. Pengine ametanguliwa na ulimi akatamka kimakosa kama mfano wa bwana yule ambaye alimpoteza mnyama wake ambapo akasema:

”Ee Allaah! Hakika wewe ni mja wangu na mimi ni mola Wako.”

Anamzungumzisha Mola wake namna hiyo kwa sababu ya furaha kubwa. Mtu anaweza kutamka kimakosa. Vilevile anaweza kuwa ni mwenye ufahamu wa kimakosa. Pia anaweza kuwa ni mjinga. Kwa hivyo ni lazima kutambua hali yake. Anatakiwa kubainishiwa. Akiendelea baada ya kubainishiwa basi hapo ndipo atahukumiwa kuwa ni kafiri.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=145451
  • Imechapishwa: 13/12/2020