ar-Raajihiy kuhusu ujinga ni udhuru 02

Swali: Ni ipi hukumu ya makafiri ambao hawakufikiwa na ulinganizi wa Kiislamu katika wakati huu au wamefikiwa kwa njia iliochafuliwa?

Jibu: Ambaye hakufikiwa basi hukumu yake ni ya wale ambao hawakufikiwa na Mtume. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَا كُنَّا مُعَذِّبِينَ حَتَّىٰ نَبْعَثَ رَسُولًا

“Hatukuwa ni wenye kuadhibu mpaka Tupeleke Mtume.”[1]

Kuhusu yule ambaye amefikiwa na ulinganizi basi amekwishasimamikiwa na hoja. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأُوحِيَ إِلَيَّ هَـٰذَا الْقُرْآنُ لِأُنذِرَكُم بِهِ وَمَن بَلَغَ

“Nimefunuliwa Wahy hii Qur-aan ili nikuonyeni kwayo na kila itakayomfikia.”[2]

Ambaye amefikiwa na hoja ya Kiislamu basi ameondokewa na udhuru.

[1] 17:15

[2] 06:19

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191047#191047
  • Imechapishwa: 29/05/2020