Swali: Je, an-Nuur ni miongoni mwa majina ya Allaah kutokana na maneno Yake (Ta´ala):

اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

”Allaah ni nuru ya mbingu na ardhi.”

Je, inafaa kusema “´Abd-un-Nuur”?

Jibu: Ibn-ul-Qayyim amesema katika “al-Qaswiydah an-Nuuniyyah” kwamba ni katika majina ya Allaah. Ametaja vilevile katika “as-Swawaa´iq” akinukuu kutoka kwa Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah kwamba ni katika sifa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Najilinda kwa nuru ya Uso wako ambayo imeangaza viza.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameomba ulinzi kutokamana na nuru ambayo ni sifa miongoni mwa sifa Zake. Sio nuru ilioumbwa. Inafaa kuitwa kwa ´Abd-un-Nuur.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com