ar-Raajihiy kuhusu jina la ´Abdun-Nuur


Swali: Ni ipi hukumu ya kuitwa kwa jina la ´Abdun-Nuur?

Jibu: Udhahiri ni kwamba hakuna ubaya. Nuru ni miongoni mwa majina ya Allaah.  Hayo yametajwa na ´Allaamah Ibn-ul-Qayyim na wengineo. Allaah (Ta´ala) amesema:

اللَّـهُ نُورُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

“Allaah ni Nuru ya mbingu na ardhi.” (24:35)

Nuru ni katika majina ya Allaah na ni miongoni mwa sifa Zake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 20/06/2021