ar-Raajihiy kuhusu hukumu ya watoto wa makafiri


Swali: Je, mtu awakatie watoto wa makafiri, mwendawazimu na watoto wa waislamu?

Jibu: Watoto wa waislamu ni wenye kuwafuata baba zao. Kuhusu watoto wa makafiri kuna maoni mbalimbali ya wanachuoni. Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ametaja katika “Twariyq al-Hijratayn” maoni yanayokaribia nane. Lakini maoni yaliyo na nguvu ni mawili:

1- Maoni ya kwanza yanasema kuwa wako Peponi.

2- Maoni ya pili yanasema kuwa watapewa mtihani.

Maoni ya sawa katika haya mawili ni kwamba wako Peponi. Dalili ya hilo ni yale yaliyothibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kisa cha ndoto ya kwamba alimuona Ibraahiym (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) akiwa pembezoni mwa watoto wa makafiri na watoto wa waislamu na kwamba si wenye kulazimishwa ´ibaadah. Maoni ya sawa ni kwamba wataingia Peponi wakifa kabla ya kubaleghe.

Kuhusu yale yanayohusiana na hukumu za duniani ni wenye kuwafuata baba zao. Kwa ajili hii wakivamiwa makafiri na kupigwa kuuawa wanauawa pamoja nao.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 01/05/2018