ar-Raajihiy josho la janaba siku ya ijumaa

Swali: Mtu akiwa na janaba siku ya ijumaa na akataka kuoga anuie josho la kuondosha hadathi kubwa au josho la ijumaa kujengea maoni yanayosema kuwa ni wajibu?

Jibu: Anuie kuondosha janaba na itamtosha kutokamana na josho la ijumaa. Akinuia josho la ijumaa, kuna tofauti kati ya wanachuoni. Akioga ijumaa peke yake na huku amesahau kuwa yuko na janaba, je, hadathi inaondoka au hapana? Maoni ya sawa ni kwamba inaondoka. Kwa sababu ni josho lililowekwa katika Shari´ah. Lakini kama atanuia kupata baridi kidogo na huku akasahau kuwa yuko na janaba hadathi haiondoki. Atakayeoga kwa ajili ya kupata baridi kidogo na yuko na janaba, je, hadathi inaondoka au hapana? Janaba haiondoki. Bali itaendelea kubaki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kila kitendo kinategemea nia na kila mmoja atalipwa kwa lile alilonuia.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (06) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/433/433.mp3
  • Imechapishwa: 08/12/2018