ar-Raajhiy kuhusu Swalaat-ut-Tasbiyh

Swali: Ni ipi Swalaat-ut-Tasbiyh ambayo mtu akiweza aiswali mara moja kwa siku au kwa wiki mara moja, na ikiwa hawezi aiswali mara moja kwa mwezi, na ikiwa hawezi aiswali mara moja kwa mwaka, na ikiwa hawezi aiswali angalau katika umri mara moja? Inaswaliwa vipi?

Jibu: Swalaat-ut-Tasbiyh ni Swalah dhaifu ambayo haikuwekwa katika Shari´ah. Haikuwekwa. Hadiyth juu yake ni dhaifu. Baadhi ya Hadiyth juu yake isnadi zake ni Swahiyh lakini hata hivyo ni Shaadhdhah zinapingana na Hadiyth ambazo ni Swahiyh. Swalah alizokuwa akiswali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mchana na usiku zimehifadhiwa. Ndani yake hamna Swalaat-ut-Tasbiyh…

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4734
  • Imechapishwa: 01/05/2015