Swali: Ikiwa mtu amepitwa katika siku ile ya saba kufanya ´Aqiyqah. Inajuzu kwake kuchinja ´Aqiyqah katika ile siku ya nane au ya tisa?

Jibu: Inajuzu, lakini lililo bora ni kuchinja katika ile siku ya tarehe ishirini na moja. Siku ya kwanza ni ile ya saba, kisha ile siku ya kumi na nne, halafu ile siku ya ishirini na moja. Haya ndio masiku bora. Vinginevyo inafaa kuchinja katika siku yoyote.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ighaathat-il-Lahfaan (74) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-25-01-1439H-01.mp3
  • Imechapishwa: 12/11/2017