´Aqiyqah kwa kubadilisha jina

Swali: Ambaye abadilisha jina lake imesuniwa kwake kuchinja kondoo wawili wa ´Aqiyqah hata kama alishafanya ´Aqiyqah ya kuchinja mwanzoni mwa kuzaliwa kwake?

Jibu: Hapana, hakuna haja. Akibadilisha jina lake hahitaji kufanya ´Aqiyqah. ´Aqiyqah ni mara moja. Kama alifanyiwa ´Aqiyqah inatosha. Hakuna juu yake kitu akibadilisha jina lake kwa jina jingine lililo bora zaidi. Hakuna ´Aqiyqah wala kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21680/هل-تجب-العقيقة-على-من-غير-اسمه
  • Imechapishwa: 11/09/2022