Swali: Ni ipi ´Aqiydah ya Ibn Siynaa? Je, alikufa katika Uislamu au katika ukafiri?

Jibu: ´Aqiydah ya Ibn Siynaa ni Ismaa´iliyyah. Hivyo ndivyo alivyosema Shaykh-ul-Islaam na akamraddi. Shaykh-ul-Islaam amemraddi vya kutosha Ibn Siynaa na kusema kuwa ni Ismaa´iliy. Baba yake alikuwa ni myahudi. Yeye Ibn Siynaa alisilimu lakini hata hivyo alikuwa akifuata madhehebu ya Ismaa´iliyyah.

Kuhusu kile alichokufa juu yake Allaah ndiye anajua zaidi. Mimi sijui.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (05) http://alfawzan.af.org.sa/node/2048
  • Imechapishwa: 27/11/2016