´Aqiydah ya Ibaadhiyyah kwa Maswahabah

Wanachuoni wa Ibaadhiyyah wanaafikiana katika kuwagawa kundi la Maswahabah wakubwa wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika mzunguko wa al-Baraa´ juu ya kwamba wao ni ufuska, giza, upotevu na usaliti. Miongoni mwa waliotiwa huko katika ngazi ya al-Baraa´ katika Maswahabah ni kiongozi mwongofu watatu ambaye ni Dhun-Nurayn ´Uthmaan bin ´Affaan, kiongozi mwongofu wanne ambaye ni ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Maswahabah wengine vigogo az-Zubayr bin ´Awwaam, Abu Muusa al-Ash´ariy, Twalhah bin ´Ubaydillaah, ´Amr bin al-´Aasw na Mu´aawiyah bin Abiy Sufyaan. Bali na Hasan bin Thaabit. Wanawaunganisha pamoja na hawa wale wanaoitwa “wenye mashaka” ambao hawakuingilia fitina ya Maswahabah na wakajitenga. Kama mfano wa ´Abdullaah bin ´Umar na Muhammad bin Salamah. Ibaadhiyyah wengi wanatangaza al-Baraa´ vilevile kwa kiongozi mwongofu, mwadilifu na mja mwema ambaye ni ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah). Bali sivyo tu, wanajitenga mbali na kila yule mwenye kumpenda. Hii ndio ´Aqiydah ya ´Ibaadhiyyah.

  • Mhusika: Abuu Swaalih Mustwafaa ash-Sharqaawiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kuntu ibaadhwiyyaa yaa layta qawmiy ya´lamuun, uk. 15
  • Imechapishwa: 11/06/2017