´Aqiydah ya at-Twabariy kwa mujibu wa adh-Dhahabiy


Ibn Jariyr amesema katika ”at-Tabsiyr fiy Ma´aalim-id-Diyn”:

“Mfano wa sifa ambazo haziwezi kutambulika kwa njia nyingine isipokuwa tu kupitia Qur-aan na Sunnah ni pale ambapo (´Azza wa Jall) anaeleza kwamba Yeye ni:

1- …  mwenye kusikia na mwenye kuona…

2- … anayo mikono miwili pale Aliposema:

بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ

“Bali mikono Yake imekunjuliwa.”[1]

3- … kwamba anao uso pale Aliposema:

وَيَبْقَىٰ وَجْهُ رَبِّكَ

”Utabakia uso wa Mola wako.”[2]

4- … kwamba ana mguu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… mpaka pale ambapo Mola ataweka mguu Wake juu yake.”

5- … kwamba anacheka. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“… mpaka pale watapokutana na Allaah hali ya kuwa anawacheka.”

6-… kwamba anashuka katika wingu la chini, kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

7- … kwamba anavyo vidole. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna moyo wowote isipokuwa uko kati ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Mwingi wa rehema.”

Maana hizi na mfano wake nilizotaja ni miongoni mwa yale Allaah aliyojisifu Mwenyewe na vivyo hivyo akamsifu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni mambo ambayo hayawezi kuthibitishwa kwa kufikiri wala kwa kuzingatia. Pamoja na hivyo hatumkufurishi yeyote ambaye ni mjinga kwazo isipokuwa baada kumsimamishia hoja.”[3]

Ahmad bin Hibatillaah ametukhabarisha: al-Hasan bin Muhammad ametukhabarisha: Abul-Qaasim al-Asdiy ametukhabarisha: Abul-Qaasim bin Abiyl-´Alaa’ ametukhabarisha: ´Abdur-Rahmaan bin Abiy Naswr at-Tamiymiy ametukhabarisha: Abu Sa´iyd ad-Daynuuriy, mshairi wa Ibn Jariyr, ametukhabarisha: Muhammad bin Jariyr at-Twabariy ametukhabarisha kuhusu ´Aqiydah yake, miongoni mwa hayo ni:

“Inamtosha mtu kuamini kwamba Mola Wake ndio Yule ambaye amelingana juu ya ´Arshi Yake. Yule mwenye kusema kinyume na hivo basi amekula patupu na kukhasirika.”

Tafsiri ya Qur-aan ya imamu huyu imejaa nukuu kutoka kwa Salaf zinazothibitisha Aayah za sifa na hazikanushi wala kuzipindisha maana na kwamba hazifanani na sifa za viumbe.

[1] 05:64

[2] 55:27

[3] Uk. 132

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/279-280)
  • Imechapishwa: 02/02/2021