Pili: Maana ya Qur-aan. al-Khaliyliy anasema alipokuwa anatoa taarifu ya Qur-aan:

“Ni maneno yaliyoteremshwa kwa herufi na maneno yake kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), miujiza kwa mpangilio na maana yake na iliyopokelewa kutoka kwake kwa njia tele kabisa kwa njia ya kukata.”[1]

Anayoyaficha al-Khaliyliy katika ufafanuzi wake wa maana ya Qur-aan atayafichua katika kurasa zinazofuata. Lakini hata hivyo tutajadili taarifu hii ili ndugu msomaji aweze kujua makosa katika taarifu ya al-Khaliyliy ili atahadhari na atahadhari vilevile na taarifu juu ya Qur-aan zilizoko katika vitabu vingine vilivyozungumzia mada hii na wanatumbukia baadhi ya wenzake wenye kuonelea kuwa Qur-aan imeumbwa pasi na wao kujua. Hayo ni katika nukta zifuatazo:

1- Katika taarifu yake hakusema kuwa Allaah amezungumza kwa Qur-aan.

2- Hakusema kuwa ni maneno ya Allaah. Alichosema ni kwamba ni maneno yaliyoteremshwa kwa herufi zake… “ Kwa nini? Jibu ni kwa kuwa yeye anapinga kutoka kwa Allaah (´Azza wa Jall) sifa ya kuzungumza. Katika ´Aqiydah ya al-Khaliyliy, kama ambavyo vilevile ndio ´Aqiydah ya Jahmiyyah, Mu´tazilah na wale wote wanaosema kuwa Quur-aan ima ni ibara au ni hikaaya/simbulizi ya maneno ya Allaah, wanasema kuwa Allaah hazungumzi si kwa Qur-aan wala kitu kingine. Wanaonelea kuwa anaumba maneno na kwamba Qur-aan na kisichokuwa Qur-aan imetengana Naye kama vilivyo viumbe vyengine vyote. Halafu anaiteremsha. Haya ndio anayokusudia al-Khaliyliy alipokuwa akielezea maana ya Qur-aan.

al-Khaliyliy anaonelea maoni ya wale wanaopinga Allaah kuwa na sifa ya kuzungumza na anasema kuwa Qur-aan imeumbwa kama viumbe wengine.

[1] Uk. 99

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 153
  • Imechapishwa: 14/01/2017