Swali: Katika nchi yetu kumejitokeza kundi linalojiita ”Answaar-ush-Shariy´ah”, wanusaraji wa Shari´ah. Mfumo wao ni wa Takfiyr na kuwashambulia wanajeshi na polisi kwa hoja kwamba hawahukumu kwa yale aliyoteremsha Allaah. Je, inajuzu kwa Ahl-us-Sunnah kushirikiana na polisi kuwapiga vita?

Jibu: Hawa hawatakiwi kuitwa ”Answaar-ush-Shariy´ah”, wanusaraji wa Shari´ah. Watu hawa ukweli wa mambo ni kwamba ni maadui wa Shari´ah. Shari´ah haihusiani na kufanya mambo ya kiajabu na kuleta tafsiri wanazotaka wenyewe na kuwakufurisha walioshikamana na haki mpaka wanachuoni mabingwa ambao wanatambulika kwa fadhilah. Hawa hawatakiwi kuitwa ”Answaar-ush-Shariy´ah”. Watu hawa wamezifanyia vibaya nafsi zao wenyewe na Shari´ah pia. Wamezifanyia vibaya nafsi zao kwa sababu ya kuwa kama walivyokuwa. Vivyo hivyo wameifanyia vibaya Shari´ah. Watu hawa wanatakiwa kulinganiwa na kubainishiwa haki. Wakimvamia muislamu, basi pasi na shaka yoyote ni sahihi kwa mtu ambaye ni mwenye dini na mwema na anahisi uzito… Huyu ni kama mfano wa jambazi. Ikiwa shari ya jambazi haiwezi kuzuiwa isipokuwa kwa kuuliwa, basi auliwe. Na ikiwa shari yake inaweza kuzuiwa pasi na kuuliwa, kama vile kwa kukamatwa na kufungwa jela, basi itatakiwa kufanya hivo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.sahab.net/forums/index.php?showtopic=141305
  • Imechapishwa: 26/09/2020