Anazingatiwa ni msafiri wa 20 km kutoka mji wake?

Swali: Mtu akitoka katika safari ya nchikavu umbali mfupi kwa mfano 20 km na amedhamiria kubaki huko nje ya nchi – je, inajuzu kwake kukusanya na kufupisha? Vivyo hivyo ikiwa safari yake ni kwenda sehemu ya mbali na wakati wa kurudi kwake akasimama nje kidogo ya nchi yake lakini hata hivyo ni masafa karibu na kwake ambapo akabaki hapo. Je, inajuzu kwake kufupisha na kukusanya?

Jibu: Ndio, inajuzu kwake kufupisha na kukusanya. Midhali ametoka nje ya nchi yake na atakaa huko nyusiku moja au nyusiku mbili ni msafiri. Kadhalika ataporudi kutoka safarini na akabaki sehemu ambayo kuna masafa mafupi na nchi yake, inafaa kwake kukusanya na kufupisha. Kwa sababu ruhusa za safari haziishi isipokuwa mpaka pale mtu anapofika katika mji wake. Kama ambavyo ruhusa za safari hazianzi isipokuwa mpaka pale mtu anapokuwa ametoka katika mji wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1419
  • Imechapishwa: 22/12/2019