Anazingatiwa ni katika wajinga si katika wanachuoni

Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa mtu wa kawaida haitakiwi kwake kujishughulisha kuyasoma mambo ya ´Aqiydah kama mfano wa Allaah kuwa juu na mengineyo?

Jibu: ´Aqiydah ndio somo muhimu zaidi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikaa akithibitisha ´Aqiydah kwa muda wa miaka kumi na tatu akiwa Makkah. Miaka yote hii ilikuwa inahusu ´Aqiydah. ´Aqiydah ndio msingi wa dini.

Swali: Mwenye kusema hivi anazingatiwa ni katika wanachuoni?

Jibu: Hapana. Hazingatiwi ni katika wanachuoni. Anazingatiwa ni katika wajinga.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 34
  • Imechapishwa: 12/06/2019