Anayolingania al-Khaliyliy yanapingana na maneno na vitendo vyake

Mwandishi Ibaadhwiy huyu amechagua maneno ambayo yana nguvu katika kuathiri kwa vile yanagonga moja kwa moja kwa kina kabisa kwenye nyoyo za wasomaji. Lakini hata hivyo mtindo huu wa kimaneno uhalisia wake ni kutaka kumpaka msomaji aliye na maumbile yaliyosalimika mchanga wa machoni. Lakini hata hivyo sio ya ukweli ambayo ni wajibu kuyasema mwanachuoni anayetafuta haki. Ni madai tu yanayoendana na maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

يَقُولُونَ بِأَلْسِنَتِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ

“Wanasema kwa ndimi zao yasiyokuweko nyoyoni mwao.”[1]

Dalili ya hilo ni kuwa mwandishi al-Khaliyliy Ibaadhwiy hakuridhia kuhukumiwa na Qur-aan na Sunnah Swahiyh zilizothibiti. Kinyume chake ameyarudisha kwa akili na matamanio yake na kusema kuhusu yaliyothibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy kupitia upokezi wa Abu Hurayrah na Abu Sa´iyd ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema wazi kabisa kuwa waumini watamuona Mola wao watapokuwa Peponi yafuatayo:

“Kuchukua udhahiri wake unarudishwa na akili na unakadhibishwa na dalili.”[2]

Huu ni ujasiri mkubwa juu ya Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 48:11

[2] Uk. 56

  • Mhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 77
  • Imechapishwa: 14/01/2017