Anayewasema Vibaya Wanachuoni Salafiyyuun Anajidhuru Mwenyewe


Swali: Hukaa na watu wanaowatuhumu wanachuoni wakubwa wa zama hizi ya kwamba ni wakali na wanafarikanisha baina ya Ummah pindi wanapowaponda na kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah wal-Firaq na makundi yaliyopo leo na kwamba wana mapungufu katika matendo na ugumu kwenye moyo kwa sababu ya haya wanayoyafanya. Je, nikae na kutangamana na watu kama hawa na ni ipi nasaha yako juu ya hili?

Jibu: Watu hawa wanazisema nafsi zao wenyewe. Madhara ya maneno haya yanawarudilia wao wenyewe na madhambi yako juu yao. Wajibu wenu nyinyi ni kuwanasihi. Wakiacha jambo hili kaeni nao. Wasipoliacha jitengeni nao na wasuseni.[1]

———
(1) Tazama http://www.wanachuoni.com/content/nasaha-tatu-tosha-kwa-anayewatukana-wanachuoni

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (07) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_07.mp3
  • Imechapishwa: 01/06/2015