Anayestahiki kunasihiwa na asiyenasihiwa wakati wa Radd

Swali: Je, ni lazima kwanza kumnasihi anayeraddiwa kabla ya Radd? Kwa sababu baadhi ya watu wanasema kuwa ni lazima kumnasihi kwanza kabla ya kumraddi. Ni ipi Manhaj ya Salaf kuhusiana na masuala haya?

Jibu: Ikiwa anakubali nasaha, bila ya shaka ni bora kuliko kumraddi. Ikiwa anakubali nasaha na atajirudi, hili ndio linalotakikana. Ama ikiwa hakubali nasaha, ni lazima kumraddi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (42) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1432-03-10.MP3
  • Imechapishwa: 16/11/2014