Swali: Tumesikia kuwa baadhi ya mawalii wa Suufiyyah mwanzoni walikuwa ni wema na wenye kufuata Qur-aan na Sunnah. Kisha wakaingiliwa na shaytwaan na kuwafitinisha kwa kuwadhihirishia mambo yasiyokuwa ya kawaida mpaka wakafikia kudhania kwamba ni katika mawalii wa Allaah ambapo fitina ikazidi kuwa kubwa na matokeo yake wakaacha kufuata Qur-aan na Sunnah. Je, hii ni dalili yenye kuonyesha kuwa mambo ya kishaytwaan yanaweza kumdhihirikia mtu anayefuata Qur-aan na Sunnah pasi na yeye kutambua hilo?

Jibu: Hapana. Hayamdhihirikii ambaye anashikamana na Qur-aan na Sunnah. Shaytwaan ni mwenye kujitenga nae mbali. Shaytwaan anachofanya ni kuwa humdanganya kwanza kuacha Qur-aan na Sunnah au humdanganya kwa kufuru. Halafu baada ya hapo sasa ndio humpitishia mambo yasiyokuwa ya kawaida ya kishaytwaan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (06) http://alfawzan.af.org.sa/node/2049
  • Imechapishwa: 06/12/2016