Anayesema hakuna tofauti kati ya waislamu na wakristo


Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusema “Hakuna kati yetu sisi na  wakristo tofauti” na anakufuru kwa hilo?

Jibu: Tunamuomba Allaah afya. Wakristo wanasema Allaah ni utatu na sisi tunasema Allaah ni Mmoja. Hakuna tofauti katika haya?! Tunamuomba Allaah afya. Ikiwa ni mwenye kukusudia kwa kusema haya, ni mwenye khatari juu ya ´Aqiydah yake. Ni lazima kwake kutubu kwa Allaah (´Azza wa Jalla).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (62) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13740
  • Imechapishwa: 16/11/2014