Anayepinga Hadiyth katika al-Bukhaariy ni kafiri?


Swali: Baadhi ya wanachuoni wamesema kwamba yule atakayepinga Hadiyth katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy basi amekufuru. Unasemaje juu ya maneno haya?

Jibu: “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy Ummah mzima wameipokea kwa kuikubali. Ni kitabu chenye kukata kabisa. Ama kuhusu kukufurishwa ni jambo linahitajia kuangaliwa vizuri. Mtu huyu anaweza kuwa amefahamu vibaya. Kwa hivyo asikufurishwe mpaka kwanza abainishiwe.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (03) http://audio2.islamweb.net/lecturs/aalrrajhee/430/430.mp3
  • Imechapishwa: 23/03/2018