Anayemtukana mtawala ni Khaarijiy


Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kuasi amri ya kiongozi au akamtukana?

Jibu: Mwenye kuasi amri ya kiongozi amemuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa hakumuamrisha maasi lakini hata hivyo akamuasi, amemuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Kuhusiana na kumtukana, haya ndio madhehebu ya Khawaarij. Wao ndio wenye kuwatukana viongozi, kuwasema vibaya na kuwachochea watu dhidi yao. Haya ni madhehebu ya Khawaarij.

Waliomfanyia uasi ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh), mabarabaro na wapumbavu wengine, walifanya hivo isipokuwa kwa sababu ya Ibn Sabaa´ khabithi myahudi. Alikuwa anaenda huku na kule na kuzungumza kwenye vikao na kuwachochea watu mpaka mwishowe watu wajinga na wapumbavu wakawa wamemfanyia uasi. Hatimae mwishoni wakamuua (Radhiya Allaahu ´anh). Ilipelekea nini katika kumuua? Kulitokea fitina kubwa kati ya Waislamu kwa sababu ya kumuua kiongozi na kufanya uasi dhidi yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (14) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_14.mp3
  • Imechapishwa: 14/06/2018