Swali: Kama inavyojulikana Salaf walikuwa wakisema “Ukimuona mtu anampenda Imaam Ahmad, Awzaa´iy na wengine mfano wao, basi tambua kuwa huyo ni mtu wa Sunnah. Mwenye kuwachukia watu hawa na watu mfano wao, basi tambua kuwa ni mtu wa Bid´ah”. Namna hii Salaf walikuwa wakiwajaribu watu kwa kuwatumia wanachuoni wa Sunnah. Kuko ambao wanasema kuwa kanuni hii haitumiki kwa wanachuoni Salafiyyuun katika zama zetu hizi. Mtu hawezi kusema kuwa mwenye kumpenda Shaykh Ibn Baaz, Shaykh Rabiy´ na watu mfano wa hawa ni mtu wa Sunnah na mwenye kuwachukia watu hawa na kuvuka mipaka yao basi ni mpotevu na sio mtu wa Sunnah. Ni yapi maoni yako kwa hilo?

Jibu: Kanuni hii inafanya kazi katika kila zama. Wale ambao wanawachukia Ahl-us-Sunnah na wale watu wanaolingania katika Sunnah, bila ya shaka ni watu wa Bid´ah.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alnajmi.net/voices.php?action=show&id=8
  • Imechapishwa: 13/09/2020