Anayefunga na kuacha baadhi ya siku Ramadhaan

Swali: Ni ipi hukumu ya yule ambaye anafunga baadhi ya siku za Ramadhaan na akaacha zengine?

Jibu: Jibu la muulizaji huyu linaweza kufahamika kutokamana na yale yaliyotangulia; nayo ni kwamba yule ambaye anafunga siku moja na akaacha kufunga siku ya kufuata hatoki katika Uislamu. Anakuwa ni mtenda dhambi mkubwa ambaye ameacha faradhi hii kubwa ambayo ni moja katika nguzo za Uislamu. Hatotakiwa kuyalipa masiku haya aliyokula kwa kuwa kuyalipa haitomfaa kitu. Haitokubaliwa kutoka kwake kutokana na yale tuliyoyaashiria punde tu ya kwamba ?ibaadah zilizowekewa nyakati maalum mtu akizitoa nje ya wakati wake uliyowekewa mpaka pasi na udhuru hazikubaliwi kutoka kwake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/81)
  • Imechapishwa: 28/05/2017