Swali: Umeshatangulia kutoa fatwa kwamba ni haramu kwa muislamu kuchukua uraia wa nchi ya kikafiri kwa sababu ina maana ya kunyenyekea kanuni zao. Je, hii ina maana kwamba mwenye kuchukua uraia wa nchi ya kikafiri anakuwa ni kafiri kama wakazi wa mji? Baadhi ya watu wanasema kuwa wewe unamkufurisha mwenye kufanya hivo.

Jibu: Sisemi kuwa ni kafiri. Mwenye kusema kuwa mimi nasema kuwa ni kafiri ni mwongo. Ninasema kuwa ni haramu na haijuzu kuchukua uraia wa nchi ya kikafiri. Idara ya Fiqh kwa miaka mingi iliyopita imethibitisha kuwa haijuzu kuchukua uraia wa nchi ya kikafiri. Anaweza kuchukua kibali cha makazi kwa kiasi cha haja yake, na sio uraia.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (40) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/ighatsah%20%20-%2028%20-%2012%20-%201436.mp3
  • Imechapishwa: 13/02/2017