Anayeacha swalah za ijumaa tatu mfululizo ni kafiri?


Swali: Inasemekana yule mwenye kupitwa na swalah za ijumaa tatu anahesabika kuwa ni kafiri. Je, maneno haya yana msingi wowote?

Jibu: Ametoa wapi maneno haya? Anamaanisha yule asiyeswali swalah ya ijumaa wala Dhuhr? Ikiwa hayo ndio makusudio ambapo mtu haswali si swalah ya ijumaa wala Dhuhr ni kweli ni kafiri. Ama ikiwa anaswali Dhuhr na si mwenye kuacha swalah hahesabiki kuwa ni kafiri. Ana makemeo ambapo Allaah ameupiga muhuri moyo wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-26-10-1434.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017