Swali: Inajuzu kwa mwanaume kumpa pete mke wake wakati wa kumchumbia au wakati wa pete au kuna kujifananisha na makafiri?

Jibu: Hii sio desturi ya waislamu. Haya yametujia kutoka kwa makafiri. Aidha pete mara nyingi inakuwa imefungamana na imani fulani. Wanaona kuwa pete zinasababisha mapenzi baina ya wanandoa. Hii ni itikadi batili. Akitaka kumpa pete ampe mbali na mnasaba wa ndoa. Anaweza kumpa pete kabla ya ndoa, baada ya ndoa, baada wamekwishahama – anaweza kumpa anachotaka. Hakuna neno.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (9) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdt–14340506.mp3
  • Imechapishwa: 03/04/2017