Anaweza kukemea maovu na asifanye hivo anapata dhambi?

Swali: Ambaye anaweza kukemea maovu na asifanye hivo anapata dhambi?

Jibu: Ikiwa anaweza na asikemee na wala asikemee mwingine anapata dhambi. Akiyakataza mmoja katika watu basi na akatekeleza wajibu basi dhambi zinadondoka kutoka kwa wengine waliobaki. Kwa sababu ni katika mambo ya wajibu kwa baadhi ya watu. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ

“Wawepo kutoka kwenu watu wanaolingania kheri na kuamrisha mema na unaokataza maovu.” (04:104)

Kukipatikana kikosa chenye kutekeleza wajibu huu basi inadondoka kutoka kwa wengine waliobaki. Asipopatikana yeyote mwenye kufanya hivo watu wote wanapata dhambi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14) https://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=audioinfo&audioid=191634
  • Imechapishwa: 18/04/2020