Swali: Ni ipi hukumu ya kuvua soksi kila wakati wa kutawadha kwa sababu ya kuhakikisha twahara?

Jibu: Huku ni kwenda kinyume na Sunnah. Huku ni kujifananisha na Raafidhwah ambao hawaonelei kujuzu kufuta juu ya khofu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia al-Mughiyrah pindi alipotaka kumvua soksi zake za ngozi:

“Ziache. Kwani hakika nilizivaa zikiwa safi.”

Akafuta juu yazo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/159)
  • Imechapishwa: 02/07/2017