Anavosema shaytwaan wakati binadamu anavosujudu

Swali 15: Je, imethibiti kwamba shaytwaan husema wakati anaposujudu binadamu:

“Ole wangu! Mwanadamu ameamrishwa kusujudu, ambapo akasujudu na atapata Pepo. Na mimi niliamrishwa kusujudu, ambapo nikakataa na ninapata Moto.”[1]?

Jibu: Haya yamepokelewa. Lakini hivi sasa sikumbuki hali ya cheni ya wapokezi wake.

Shaytwaan hujiombea maangamivu anapomuona mwanadamu anasujudu na atapata Pepo. Na mimi niliyekataa nitapata Moto. Kusema kwamba shaytwaan alikataa kinachoasiriwa ni pindi Malaika walipomsujudia Aadam ambapo shaytwaan akakataa.

[1] Muslim (82).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 33
  • Imechapishwa: 03/10/2018